>> PAMBANO LA SIMBA, AZAM LAINGIZA MIL 64/-
PATA ZAIDI:
Release No. 186
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Oktoba 29, 2013
PAMBANO LA SIMBA, AZAM LAINGIZA MIL 64/-
Pambano la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya
Simba na Azam lililochezwa jana (Oktoba 28 mwaka huu) Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam limeingiza sh. 64,261,000.
Washabiki waliohudhuria mechi hiyo namba
76 iliyomalizika kwa Azam kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 walikuwa
10,728 ambapo viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh.
20,000.
Mgawo wa mapato hayo ulikuwa kama
ifuatavyo; Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 9,802,525.42, gharama
za kuchapa tiketi sh. 3,793,490 wakati kila klabu ilipata sh.
14,946,170.45.
Wamiliki wa uwanja walipata sh.
7,599,747.49, gharama za mchezo sh. 4,599,848.61, Bodi ya Ligi sh.
4,599,848.61, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh.
2,279,924.31, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh.
1,773,274.46.
SIMBA,KAGERA SUGAR KUKUTAANA LEO ALHAMISI
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inaanza raundi
ya 12 Leo (Oktoba 31 mwaka huu kwa mechi kati ya Simba na Kagera
Sugar itakayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10
kamili jioni.
Viingilio katika mechi hiyo
itakayooneshwa moja kwa moja na Azam Tv kupitia TBC 1 vitakuwa sh.
5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 kwa VIP A.
Nayo Yanga itashuka uwanjani Novemba
Mosi mwaka huu katika mechi nyingine ya ligi hiyo dhidi ya JKT Ruvu
itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Novemba 2 mwaka huu kutakuwa na mechi
nne; Mgambo Shooting na Coastal Union (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga),
Tanzania Prisons na Oljoro JKT (Uwanja wa Sokoine, Mbeya), Azam na Ruvu
Shooting (Azam Complex, Dar es Salaam), na Mtibwa Sugar na Rhino Rangers
(Uwanja wa Manungu, Morogoro).
Raundi hiyo itakamilika Novemba 3 mwaka
huu kwa mechi moja ambapo Mbeya City itakuwa mwenyeji wa Ashanti United
kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
Mechi za kukamilisha mzunguko wa kwanza
wa ligi hiyo zitachezwa Novemba 6 na 7 mwaka huu. Novemba 6 ni JKT Ruvu
vs Coastal Union, Ashani United vs Simba, Kagera Sugar vs Mgambo
Shooting, Rhino Rangers vs Tanzania Prisons na Ruvu Shooting vs Mtibwa
Sugar.
Novemba 7 mwaka huu, Azam itacheza na Mbeya City wakati Yanga itacheza na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Wambura Mgoyo
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)