Mtafiti
wa maswala ya kijamii kutoka Mtandaowa jinsia Tanzania(TGNP), Dinah
Nkya,akitoa mada katika semina ya waandishi wa habari kutoka Kanda ya
Nyanda za juu kusini.
Afisa uhusiano wa TGNP, Melkizedeck Karol akiendesha mafunzo ya siku mbili kwa waandishi wa habari.
Waraghibishi
kutoka kituo cha maarifa na taarifa cha Tuamke, Nsalaga wakiwa kwenye
chumba cha semina baada ya kutoa mambo mbali mbali waliyoyafumbua kutoka
vijijini.
Waandishi wa habari wakishiriki semina hiyo.
IMEELEZWA
kuwa iwapo wanawake wataendelea kuwa nyuma katika kuwania
nafasi mbali mbali za uongozi ikiwemo Urais bado changamoto
zilizopo katika jamii zitaendelea kuwatesa wanawake nchini.
Kauli
hiyo imetolewa na ofisa mawasiliamo wa mtandeao wa Jinsia
Tanzania(TGNP) Melikizedeck Karol wakati akitoa mada ya ushiriki
wa wanawake kwenye uchaguzi mkuu mwaka 2015 wakati wa mafunzo ya
siku mbili ya wanahabari mikoa ya nyanda za juu kusini.
Yaliyofanyika jijini Mbeya.
Alisema
kuwa usawa katika nafasi za uongozi wa kutaka kuwa na asilimia 50
kwa 50 kati ya wanawake na wanaume ni lazima utimie katika
uchaguzi huu kwa wanawake kuanza kujitokeza kuwania nafasi mbali
mbali zikiwemo za juu kama Urais ,ubunge na udiwani .
Hata
hivyo Ofisa huyo alisema kwamba mwaka 2005 kuwa akidi nzima ya bunge
la jamhuri ya muungano wa Tanzania ni wabunge 357 kwa mujibu wa
katiba hata hivyo viti maalum pekee ni 102 sawa na asilimia 28.6
vilivyogawanywa miongoni mwa vyama vya siasa kwa kuzingatia matokeo
ya uchaguzi kati ya viti 239 vya majimbo (vikiwemo kutoka Zanzibar) ni
wanawake 21 tu sawa na asilimia 8.8 ndio walipewa viti vya
kuchaguliwa bungeni.
Alisema
ili kuwepo na usawa hakuna budi kwa wanawake kujitokeza kwa wingi
kugombea nafasi za uongozi ikiwemo urais katika uchaguzi mkuu
unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.
"Hivi
wataka kusema hakuna mwanamke katika nchi hii ambae anaweza
kuongeza nchini kama Rais na kama wapo kwanini hawajitokezi kugombea
nafasi za juu kama Urais .....lazima wanawake wachangamkie nafasi
hiyo "
Alisema
kwa mwaka 2005 kuwa akidi nzima ya bunge la jamhuri ya muungano wa
Tanzania ni wabunge 357 kwa mujibu wa katiba hata hivyo viti
maalum pekee ni 102 sawa na asilimia 28.6 vilivyogawanywa miongoni mwa
vyama vya siasa kwa kuzingatia matokeo ya uchaguzi kati ya viti 239
vya majimbo (vikiwemo kutoka Zanzibar) ni wanawake 21 tu sawa na
asilimia 8.8 ndio walipewa viti vya kuchaguliwa bungeni.
Huku
idadi ya madiwani wa kuchaguliwa asilimia 4 na wenyeviti wa
vijiji ni asilimia 2 wakati wenyeviti wa vitongoji ni asilimia 3 .
Hivyo
alisema ni wajibu kwa vyombo vya habari na wanawabari nchini
kuendelea kuhamasisha makundi ya vijana na wanawake kujitokeza
kwa wingi katika nafasi za udiwani ,ubunge na Urais katika uchaguzi
mkuu mwaka huu.
Na Mbeya yetu Blog