MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

Monday, 15 December 2014

Genevieve Nnaji aeleza sababu za kutokua kwenye ndoa


gene
Mwigizaji wa Nollywood Genevieve Nnaji amefunguka kuhusu hatma ya maisha yake ya ndoa na kuelezea ni kwa nini hana haraka ya kuingia katika maisha hayo kwa sasa.
Kwa mujibu mahojiano aliyofanyiwa na Gazeti la Vanguard la Nigeria amesema ndoa sio kitu cha kukurupuka na kinahitaji muda zaidi katika kujipanga na kutekeleza.
“Endapo nitaolewa,natamani sana nidumu kwenye ndoa yangu na kudumu kwake najua si kazi ndogo inahitaji uvumilivu mkubwa,nafahamu unapoingia unatakiwa kufahamu kile ni kifungo cha moja kwa moja na mwenzako ndio wa kufa na kuzikana hivyo tunapaswa kutambua kuna shida na raha zake na pia tunapaswa kujifunza kusamehe na kusahau endapo tunakwazana na wenza wetu,”alisema Genevieve.

Jaji anakamatwa na dawa za kulevya wakati akiendesha kesi mahakamani


law
Mwanasheria nchini Marekani amefunguliwa mashtaka baada ya kukutwa na kete za dawa za kulevya aina ya Heroine wakati akienda kesi.
Dawa hizo  zenye thamani ya dola za kimarekani 30,000 zilikutwa katika bahasha yenye kadi ndani wakati akisoma mashtaka.
Jaji huyo mwenye miaka 63 Stephen Beecher atahukumiwa katika mahakama za juu  na huenda akatumia kifungo cha miaka miwili kutokana na kosa la kuingiza dawa za kulevya mahakamani.
Kwa mujibu wa uchunguzi wa polisi walidai dawa hizo ambazo walizikuta zimefungwa ndani ya bahasha iliyokua na kadi ndani yake wakati akijaribu kuziiba na zilitoka kwa mmoja wa watuhumiwa waliokamatwa wakati wakijaribu kuzisafirisha na zilikua zikisubiri ushahidi wakati kesi ikitarajiwa kusikilizwa wakati wowote.

Mwakilishi wa South Africa, Rolene Strauss A twaa Taji la Miss World 2014,


Jana December 14 kwenye Historia ya mwaka 2014, Mashindano makubwa ya Miss World 2014yalikuwa yakifanyika London, Uingereza ambapo washiriki mbalimbali ikiwa ni pamoja na mwakilishi wa Tanzania, Happiness Watimanywa akiwa mmoja ya washiriki hao.
Mpaka leo asubuhi matokeo ya kura ambazo zilikuwa zikipigwa na watu zilimuweka mwakilishi huyo kuwa katika nafasi ya pili, akitanguliwa na Miss Thailand ambapo iwapo Happiness angekuwa namba moja basi ilikuwa moja kwa moja aingie kwenye Top 10 ya mashindano hayo.
Kutokana na Hapiness kupitwa kura na Miss Thailand hakufanikiwa kuingia kwenye Top 10, huku katika wale waliotajwa ni wawakilishi wawili pekee, mmoja wa South Africa na mwakilishi wa Kenya waliofanikiwa kuingia Top 10.
Mwakilishi wa South Africa, Rolene Strauss amefanikiwa kuvuka hatua zote na hatimaye kutangazwa mshindi wa Taji la Miss World 2014, nafasi ya pili ikishikwa na Miss Hungary, Edina Kulcsar na nafasi ya tatu kushikwa na Miss USA, Elizabeth Safrit.
Hapa nimekuwekea picha za matukio yote ya sherehe hizo.

Mgombea Uenyekiti Chama cha CCM amefariki dunia gafla muda mfupi baada ya kupiga kura.


 



MWANANCHI
Mgombea Uenyekiti kupitia Chama cha CCM Mtaa wa Swea kata ya Mkolani Mwanza Pius Mihayo amefariki dunia gafla akiwa mtaani kwake muda mfupi baada ya kupiga kura.
Msimamizi wa uchagyzihuo Halifa Hida alisema mgombea huyo alifariki dunia gafla akiwa kwenye mtaa wake wa Swea na chanzo cha kifo chake hakijajulikana.
“Sasa kwa mujibu wa taratibu za uchaguzi,tutatangaza matokeo ya wajumbe na nafasi za wagombea wa vitimaalum,nafasi ya uenyekiti haitatangazwa hadi taratibu nyingine za uchaguzi zitakapoandaliwa”alisema Hida.
Mkoani Arushamsongamano wa wapigakura katika kituo chaMbauda kata ya Sombetini unadaiwa kusababisha kifo cha mtu aliyetambulika kwa jina la Suleiman Bakari.
Tukio hilo lilitokea saa 3 asubuhi katika kituo hicho ambacho kilikua kimefurika watu ambapomtu huyo alianguka gafla baadaya kukosa hewa akiwa kwenye mstari wa kupigakura.
NIPASHE
Uchaguzi wa Serikali za mitaa,vijiji na vitongoji ulifanyika nchini kote jana huku ukitawaliwa na kasoro na vurugu kubwya  zilizosababishapolisi kutumia risasi za moto na baadhi ya wapigakura kuchapana makonde jijini Dar es salaam.
Vurugu hizo zilitokana na uchaguzi huo kugubikwa na kasoro nyingi na hivyo kusababisha baadhi ya vituo kulazimika kuahirisha uchaguzi huo hadi wiki ijayo.
Baadhi ya kasoro zilizoibuka zilitokana na baadhi yavituo kuchanganya majina ya wagombea,kuchelewa kuanza kwa uchaguzi,kukosekana kwa vifaa vya kupigia kura pamoja na baadhi ya wagombea kuwahujumu wengine.
Uchaguzi huo ulipangwa kuanza saa2 asubuhi lakini maeneo mengi ulichelewa kuanza kutokana na vifaa kuchelewa kufika vituoni.
Katika kituo cha Kimara bucha kulitokea vurugu kubwa baada ya mawakala kugombea kuwasaidia wapigakura kuweka alama ya vyema kwa wagombea na baadhi ya watu kutaka kurudia kupiga kura hali iliyosababisha msimamizi wa kituo hicho kupigwa na wapigakura kutokanana na kukerwa na kitendo cha baadhi yawatu kurudia kupiga kura.
NIPASHE
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Stephen Masele ambaye pia ni Mbunge wa Shinyanga mjini amevamiwa na kundi la vibaka wakati akienda Zahanati kupatiwa matibabu na kisha kuporwa vitu mbalimbali mjini Shinyanga.
Masele alisema tukio hilo lilitokea juzi saa4 usiku wakati akienda kupatiwa matibabu ya matatizo ya koo katika Zahanati ya Bakwata  na gafla alivamiwa na kundi la watu wapatao 30 na kumpora mali zake.
Alisema akiwa na Naibu Katibu mkuu CCM Zanzibar,Vuai Aly wakipata chakula cha usiku hotelini gafla alijisikia vibaya na kuamua kwenda kwenye Zahanati hiyo kupatiwa matibabu na ndipo alipata mkasa huo wakati akiwa njiani.
Masele alikanusha tuhuma alizozushiwa na wananchi kuwa kuporwa huko kunatokana na yeye kugawa rushwa kwa wananchi wakati wa kampeni Serikali za mitaa ili wananchi wawachague wagombea wa CCM.
MTANZANIA
Katibu wa CCM kata ya Narungombe Lindi Mohamed Pilipili amevamiwa na kupigwa hadi kuzimia na mabaunsa kwa madai ya kufanya kampeni ya nyumba kwa nyumba usiku.
Tukio hilo lilitokea juzi usiku katika kitongoji cha Chikwale baada ya kundi la mabaunsa kumvamia na kumpiga Katibu huyo pamoja na Mwenyekiti wa CCM wa kata hiyo Seleman Lukuche.
Akizungumzia tukio hilo Lukeche alisema ilikua saa 3 usiku wakitoka Ruangwa kupeleka taarifa za mwenendo wa uchaguzi pamoja na majina ya mawakala wa CCM ndipo walipovamiwa na kundi hilo la mabaunsa10waliodai wao wanadhibiti .vitendo vya rushwa ambao walianza kuwapiga bila kutaka maelezo.
Katika tukio jingine mgombea wa nafasi ya uenyekiti kata ya Mkwajuni amepigwa na watu wanaodaiwa wafuasi wa CUF kwa madai kuwa alikwenda kwenye eneo la Mjimwema kupanga mikakati ya kuiba kura.
UHURU
Muda wowote kuanzia sasa Rais Jakaya Kikwete atatoa na kutangaza uamuzi wake kuhusiana na baadhi ya watendaji wakiwemo Mawaziri kuhusishwa katika kashfa ya wizi wa fedha za Tegeta Escrow.
Wiki iliyopita Rais alipokea na kupiia ripoti iliyowasilishwa kwake,nyaraka na ushauri uliotolewa katika maazimio ya Bunge kuhusu akaunti ya Tegeta Escrow.
Kikwete ambaye alianza kazi Desemba 8 mwaka huu baada ya mapumziko kutokana na kufanyiwa upasuaji alisema atatoa uamuzi wake ndani ya wiki hii.
Alisema atatolea maamuzi mambo ambayo yanamuhusu yeye moja kwa moja na yale yanayohusu Serikali atatolea uamuzi na maelekezo ya namna ya kuyashughulikia.
Bunge lilitoa maazimio mbalimbali kwa Serikali ikiwemo kuitaka mamlaka ya uteuzi  kuwawajibisha ikiwani pamoja na kuwavua nyadhifa zao Waziri wa Nishati na Madini,Mwanasheria mkuu,Waziri wa nyumba na maendeleo ya makazi,Katibu mkuu wa Wizara ya Nishati na madini na wengineo.
HABARILEO
Kundi la watu wanaodhaniwa kuwa majambazi wamevamia na kupora fedha na vitu mbalimbali ndani ya kanisa Katoliki la Kilema jimbo la Moshi vijijini Mkoani Kilimanjaro.
Tukio hilo lilitokea usiku wa kuakia jana ambapo watu hao wakiwa na vifaa maalum  vya kuvunja milango,walivunja langokuu la kanisa hilo na kuvunja sanduku la sadaka na kupora vifaa vya kufanyia ibada.
Padri wa Parokia ya Kilema Damian Temere alisema vitu vilivyoibwa ni pamoja na vifaa vitakatifu vinavyotumika katika sikukuu ya Ekaristi na majambazi hayo yalivunja kasha la kuhifadhia sadaka na kupora fedha zilizokuwemo ambazo hazikujulikana thamani yake.
Alisema pia waliiba vifaa vya kunywea divai na kumunio ambavyo nivya dhahabu vyenye thamani ya mamilioni ya fedha huku wakiacha vile vya shaba.
Alisema baadhi ya vifaa hivyo vilinunuliwa na wamisionari wa kwanza na vilikua na thamani kubwa kwa kanisa hilo kwa kuwa niliwakilisha imani katika parokia hiyo na kanda nzima ya Kaskazini.
MWANANCHI
Shirika la usafiri wa anga la China Avic International liko kwenye mazungumzo na Shirika la ndege la hapa nchini ATCL ili kuliwezesha Shirika hilo la Tanzania kufanya kazi kwa ufanisi.
Avic inayomilikiwa na Serikali ya China imesema mkakati wake wa kwanza ni kutoa ndege kwa ATCL ili kuboresha huduma zake,kufanya kazi na kujiendesha kama ilivyo kwa mashirikayandege ulimwenguni.
Naibu Katibu mkuu wa Wizara ya UchukuziMonica Mwamunyange alisema kituo hicho kimeanzishwa baada ya makubaliano ya nchi mbili yaliyofanyika China mwezi Oktoba mwaka huu wakati Kikwete alipotembelea nchi hiyo.
“Tuliangalia suala la kuunganisha nguvu kati ya ATCL na Avic International na tayari wenzetu wa China wameamua kuanzisha kituo hiki”alisema Mwamunyange.

HANSPOPE ASEMA YANGA NI TIMU MBOVU


MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hanspope amesema kikosi cha Yanga SC walichokichapa mabao 2-0 jana ni kibovu, hivyo wana kazi ya ziada kuhakikisha wanakuwa na timu imara zaidi.
Simba SC iliifunga Yanga SC mabao 2-0 katika mechi ya Nani Mtani Jembe 2 iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jana jioni. Shukrani kwa mabao ya kiungo Awadh Juma na mshambuliaji Elias Maguri waliyoyafunga kipindi cha kwanza.
Hanspope ameuambia mtandao huu kuwa kikosi cha Simba SC kilicheza vizuri lakini hawapaswi kubweteka kwa sababu wamepata ushindi na kucheza soka zuri dhidi ya timu iliyokuwa mbovu ya Yanga SC.
POPPE
“Tulicheza vizuri lakini tulicheza na timu mbovu. Yanga hawako vizuri, tungepata ushindi dhidi ya timu bora tungejivunia. Zipo timu nzuri msimu huu kama Mtibwa Sugar na si Yanga hawa wabovu,” amesema Hanspope.”
Sisi (Friends of Simba) tumechukua timu ili tuipe mafanikio, hatujachukua timu ili tuiharibu. Tunawaomba wanasimba watupe muda na watuamini tuitengeneze hii timu,” amesema zaidi Hanspope.
Yanga SC pia ilifungwa mabao 3-1 na Simba SC katika mechi ya kwanza ya Nani Mtani Jembe iliyochezwa Uwanja wa Taifa Desemba 21 na kupelekea kufukuzwa kwa benchi zima la ufundi la Yanga.
Mabao ya Simba SC yalifungwa na mshambuliaji Mrundi Amissi Tambwe aliyefunga mara mbili na kiungo Awadh ambaye ameweka rekodi ya kufunga katika mechi ya Nani Mtani Jembe. Bao pekee la Yanga SC lilifungwa na mshambuliaji Emanuel Okwi ambaye hata hivyo amerudi katika timu yake ya Simba SC.

Na Bertha Lumala, Dar es Salaam

MWAMBUSI AMTOLEA MACHO HAMISI KIIZA BAADA YA KUTEMWA NA YANGA


Kocha wa Mbeya City, Juma Mwambusi ameonekana akipiga stori na Hamisi Kiiza wa Yanga.

Mwambusi alifanya hivyo wakati Yanga na Simba wakipambana kwenye Nani Mtani Jembe kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.

Mazungumzo yao yalionyesha yakisisitiza jambo huku Kiiza ambaye ametemwa Yanga kumpisha Mliberia, Kpah Sherman akielezea kitu fulani kwa muda mrefu.

Alipoulizwa Mwambusi kama ilikuwa ni sehemu ya kumshawishi Mganda huyo kutua Mbeya City, yeye alisisitiza hakuwa yeye.


“Mimi! Sijazungumza na Kiiza labda umenifananisha,” alisema.
Lakini taarifa zilizopo  kutoka chanzo chetu cha habari kinasema mwambusi amemtoleo macho kiiza na inawezekana akatua mbeya city na hii nia taarif ya siri  lani mtandao huu umekupa kipande tu cha stori hii

TAMBWE AITWA NA VITAL'O BAADA YA SIMBA KUMTUPIA VIRAGO,



Baada ya Simba kumtema, mshambuliaji Amissi Tambwe anaanza kujiandaa kurejea kwao Burundi.

Tambwe amemuambia rafiki wake wa karibu kwamba anarejea na kujiunga na timu yake ya zamani ya Viral’O.

“Amesema Vital’O wamemuita, hivyo anachosubiri ni kumalizana na Simba kuhusiana na haki zake,” alisema rafiki huyo wa Tambwe.


Tambwe alitokea Vital'O na kujiunga na Simba, wakati akiichezea timu hiyo ya Burundi alikuwa mfungaji bora wa Burundi pia michuano ya Cecafa.

Lakini alipoulizwa Tambwe akasema atazungumza baadaye kidogo kwa kuwa kuna watu anataka kumalizana nao. Sijui ni akina nani?

SERENA WILLIAM AANZA MAZOEZI KWA KUJIANDAA NA MSIMU UJAO


Mcheza tenisi namba moja duniani, Serena Williams ameanza mazoezi kujiandaa na msimu ujao kwa kufanya michango.


Serena alifanya hivyo katika mbio maalum zilizofanyika Florida Miami, Marekani na fedha zilizochangishwa wakati wa mbio hizo zilikwenda kwenye Serena William Fund.

Watu mbalimbali walijitokeza kukimbia kilomita tano pamoja na robo Marathoni.
Mmoja wa waliojitokeza ni dada yake, Venus William.


Sunday, 14 December 2014

ANgalia watu alio zimia jana katika mechi ya nani mtani jembe jana

 







SIMBA leo imeendeleza ubabe dhidi ya Yanga katika mchezo wa Kampeni ya Nani Mtani Jembe baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mchezo kama huo Desemba 21 mwaka jana Simba iliibuka na ushindi wa mabao 3-1, yaliyofungwa na Amis Tambwe na Awadh Juma.

Mchezo huo ulichezeshwa na mwamuzi Jonesia Rukyaa, ikiwa ni mara ya kwanza katika historia mechi ya Simba na Yanga mwanamke kupuliza filimbi.

Mfungaji wa bao la tatu katika mchezo kama huo mwaka jana, Awadhi Juma, ndiye jana alifunga bao la kwanza dakika ya 30 akimalizia mpira wa adhabu uliopigwa na Emmanuel Okwi na kutemwa na kipa Deogratius Munishi ‘Dida’.

Bao hilo lilionekana kuwachanganya sana wachezaji wa Yanga na kujikuta wakicheza hovyo, hali iliyosababisha wafungwe bao la pili dakika ya 40, mfungaji akiwa Elius Maguli.

Maguri alifunga bao hilo baada ya mpira wa kichwa aliopiga kugonga nguzo ya goli na kurejea uwanjani na kumkuta mfungaji aliyeukwamisha wavuni na kumuacha Dida akigaagaa.

Yanga ingeweza kupata bao la mapema kutokana na kufanya mashambulizi ya kushtukiza baada ya kuanza mchezo huo, lakini umalizijia haukuwa mzuri.

Mshambuliaji mpya wa Yanga, raia wa Liberia, Kpah Sherman mara kadhaa alijaribu kufurukuta lakini alikosa ushirikiano wa kutosha.


Simba nayo licha ya ushindi huo, lakini washambuliaji wake wakiongozwa na Simon Sserunkuma, Elias Maguli na Emmanuel Okwi walipata nafasi za kufunga, lakini walishikwa na kigugumizi cha miguu kila waliposogea eneo la hatari.

Kipindi cha pili, Yanga ilipata pigo baada ya Sherman kuumia, hivyo kutolewa nje na nafasi yake kuchukuliwa na Mrisho Ngassa.

Dakika ya 62, Danny Mrwanda aliyeingia kipindi cha pili badala ya Andrey Coutinho nusura aipatie Yanga bao, baada ya mpira aliopiga kuokolewa na beki Hassan Isihaka, wakati kipa Ivo Mapunda hayupo golini.

Dakika ya 67 Sserunkuma akiwa katika nafasi nzuri ya kufunga, shuti lake lilipaa juu kidogo ya lango la Yanga, huku tayari baadhi ya mashabiki wa Simba wakianza kuinuka wakiamini amefunga.

Simba: Ivo Mapunda, Nassor Masoud, Mohammed Hussein/Issa Rashid,
Hassan Isihaka,  Juuko Murishid/Joseph Owino, Jonas Mkude, Ramadhani Singano/Said Ndemla, Awadh Juma, Elius Maguri/Danny Sserunkuma, Simon Sserunkuma/Shaaban Kisiga na Emmanuel Okwi.

Yanga: Deogratius Munishi, Abdul Juma/Hussein Javu,Oscar Joshua, Nadir Haroub, Kelvin Yondani, Mbuyu Twite/Hassan Dilunga, Haruna Niyonzima, Emerson Roque/Salum Telela, Simon Msuva, Kpah Sherman/Mrisho Ngassa na  Andrey Coutinho/Danny Mrwanda.

Saturday, 13 December 2014

Angalia Walioshinda Tuzo za TASWA 2013/2014 hapa,


gold-star-award-375x250Siku ya jana December 12 kulikuwa na Sherehe za Utoaji wa Tuzo za Wanamichezo Bora Tanzania mwaka 2013/2014, zilizotolewa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) ambazo zilifanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, ambapo Mgeni Rasmi katika Sherehe hizo alikuwa Rais Wa Zanzibar, Dr. Ali Mohamed Shein
Tuzo kubwa ya kwanza iliyotolewa usiku wa jana ni Tuzo ya Heshima ambayo ilitolewa kwa Hayati Sheikh Abeid Aman Karume na kupokelewa na Mama Fatma Karume.
Sheridah Boniface alivunja Rekodi kwenye sherehe hizo baada ya kutoka na jumla ya Tuzo tatu, Tuzo ya Jumla ya Mwanamichezo Bora 2013/ 2014, tuzo ya Mwanamichezo Bora Chipukizi na Tuzo ya Mchezaji Bora wa Soka Wanawake.
Wachezaji wa Azam, Erasto Nyoni na Kipre Cheche baada ya kupokea tuzo zao.
Wachezaji wa Azam, Erasto Nyoni na Kipre Cheche baada ya kupokea tuzo zao.
Tuzo ya Mchezaji Bora wa Gofu Wanawake imechukuliwa na Madina Iddy.
Tuzo ya Mchezaji Bora wa Gofu imechukuliwa na Nuru Mollel.
Tuzo ya Mchezaji Bora wa Gofu Wanawake imechukuliwa na Madina Iddy.
Tuzo ya Mchezaji Bora wa Gofu ya Kulipwa imechukuliwa na Hassan Kadio.
Tuzo ya Mchezaji Bora Mpira wa Kikapu Wanaume imechukuliwa na Lusajo Samweli.
Tuzo ya Mchezaji Bora Mpira wa Kikapu wanawake imechukuliwa na Sajda Ahmed Lyaimaga.
Tuzo ya Mchezaji Bora Mpira wa Wavu Wanaume imechukuliwa na Kelvin Peter Severino.
Tuzo ya Mchezaji Bora Mpira wa Wavu Wanawake imechukuliwa na Teddy Abwao.
Tuzo ya Mchezaji Bora Mpira wa Magongo Wanaume imechukuliwa na Yohana Wilson.
Tuzo ya Mchezaji Bora Mpira wa Magongo Wanawake imechukuliwa na Kidawa Seremala.
Tuzo ya Mchezaji Bora wa Soka Wanaume imechukuliwa na Erasto Nyoni.
Tuzo ya Mchezaji Bora wa Tenisi Walemavu imechukuliwa na Novatus Emmanuel Temba kwa upande wa Wanaume.
Tuzo ya Mchezaji Bora wa Tenisi Walemavu imechukuliwa na Rehema Selemani Saidi kwa upande wa Wanawake.
Tuzo ya Mchezaji Bora wa Olimpiki Maalum imechukuliwa na Blandina Blasi kwa upande wa Wanawake.
Tuzo ya Mchezaji Bora wa Olimpiki Maalum imechukuliwa na Raphael Kalukula kwa upande wa Wanaume.
Tuzo ya Mchezaji Bora wa Nje anayechezea Tanzania imechukuliwa na Kipre Cheche.
Tuzo ya Mchezaji Bora Mtanzania anayechezea nje imechukuliwa na Mbwana Samatta.
Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mpira wa Mikono Wanaume imechukuliwa na Hemed Saleh.
Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mpira wa Mikono Wanawake imechukuliwa na Veronica Mapunda.
Tuzo ya Mwendeshaji Bora wa Baiskeli imechukuliwa na Richard Laizer kwa upande wa wanaume.
Tuzo ya Mwendeshaji Bora wa Baiskeli imechukuliwa na Sophia Adson kwa upande wa wanawake.
Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ngumi za Ridhaa imechukuliwa na Bondia Suleiman Kidunda.
Tuzo ya Mchezaji Bora wa ngumi za Kulipwa imechukuliwa na Bondia Francis Cheka.
Tuzo ya Mchezaji Bora wa Tenisi Wanaume imechukuliwa na Omary Sulle.
Tuzo ya Mchezaji Bora wa Tenisi Wanawake imechukuliwa na Rehema Athumani.
Tuzo ya Mchezaji Bora wa Kike mchezo wa Judo imechukuliwa na Grace Alfonce Mhanga.
Tuzo ya Mchezaji Bora wa Kiume mchezo wa Judo imechukuliwa na Geofrey Edward Mtawa.
Tuzo ya Mwanariadha Bora wa Kike imechukuliwa na Zakia Mrisho.
Tuzo ya Mwanariadha Bora wa Kiume imechukuliwa na Alfonce Felix.
Tuzo ya Muogeleaji Bora wa Kike imechukuliwa na Catherine Maswa.

LIVE KUTOKA TAIFA;...YANGA 0 VS SIMBA 2 (FULL TIME)

 

MPIRA UMEKWISHAAAAAAAAAA
Dk 89, Mrwanda anaangushwa, Niyonzima anapiga lakini Ivo anadaka kiulaiiinii

Dk 87, mashabiki Yanga wanaanza kutoka uwanjani, Simba wanawazomea
Dk 86, Simba wanamtoa Simon Sserrunkuma na kumuingiza Shabani Kisiga

Dk 84 Simba wanamtoa Maguri, nafasi yake inachukuliwa na Danny Sserunkuma. Mwamuzi anampa Maguri kadi ya njano kwa kupoteza muda
Dk 78 Yanga inamtoa Juma Abdul na kumuingiza Javu

Dk 76, Ngassa anapiga krosi lakini inaishia mikononi mwa Ivo Mapunda

Dk 72, Simba wanamtoa Messi na nafasi yake inachukuliwa na Said Ndemla
Dk 65, Simba wanamtoa Tshabalala Mohammed Hussein aliyeumia, nafasi yake inachukuliwa na Issa Rashid 'Baba Ubaya'
Dk 66, Mrwanda anapiga mpira langoni kukiwa na mabeki tu, Owino anaruka juu na kuokoa kwa kichwa.

Dk 65 Yanga wanamuingiza Mrisho Ngassa kuchukua nafasi ya Mliberia Sherman aliyeumia

Dk 63, Mliberia Sherman anatoka nje mwenyewe baada ya kuumia. Awali alirudi, lakini anaonekana kuzidiwa
Dk 56, Yanga inamuingiza Salum Telela na kumtoa Mbrazil, Emerson

Dk 52 Yondani anafanya kazi ya ziada kuokoa mpira mbele ya Messi Singano. Simba bado wanatawala katikati ya uwanja

Dk 49, Sherman anawaacha mabeki wa Simba, wanamuangusha, inakuwa faulo inayookolewa na mabeki wa Simba
Dk 48, Msuva anapiga shuti kali lakini mpira unazuiwa
Dk 46 Simba wanamtoa Murishi wanamwingiza Joseph Owino
          Yanga wanamtoa Coutinho wanamwingiza Danny Mrwanda
MAPUMZIKO
GOOOOOOOO Dk 41 Maguri anaifungia Simba bao baada ya kuunganisha mpira wa kurusha wa chollo ambao uligonga mwamba, mabeki wa Yanga wakazubaa, akarudi na kufunga tena.


Dk 40, Yanga wanamtoa Twite aliyeumia, nafasi yake anachukua Hassan Dilunga

Dk 33, Coutinho anapiga shuti saafi lakini linatoka nje sentimeta chache

GOOOOOOOOOOOOO DK 30, Awadhi Juma anauwahi mpira wa faulo wa Okwi na kuukwamisha wavuni ilikuwa ni baada ya Dida kuutema.

Dk 25 Sherman anampa pasi nzuri Msuva naye anaachia shuti kali lakini linapiga nyavu za nje.

Dk 23, Sherman anagongeana vizuri na Msuva na kutoa pasi nzuri....lakini hakuna mmaliziaji
Dk 17, Okwi anawachambuamabeni wawili wa Yanga lakini anaangushwa na kuwa faulo, anaipiga Okwi...goal kick

Dk 13 vurugu zinazuka, lakini mwamuzi anachukua maamuzi magumu na kutotoa kadi...ubabe unatawala
Dk 11 Emerson anapiga krosi safi lakini Coutinho anaukosa mpira
Dk 7, Sherman anawachambua mabeki watatu wa Simba lakini anashindwa kumalizia


Dk 5, Sserunkuma Jr anatolewa nje anatibiwa baada ya kugongwa na Yondani
Dk 3, Yanga wanafanya shambulizi, Sherman anampa pasi nzuri Msuva anapiga shuti linadkwa na Ivo

Dk 2, Okwi anapiga mkwaju wa faulo lakini unadakwa vizuri na Dida.

VIKOSI VYA LEO YANGA VS SIMBA
YANGA:
Deo Dida
Abdul Juma
Oscar Joshua
Nadir Haroub
Kelvin Yondani
Mbuyu Twite
Haruna Niyonzima
Emerson Roque
Simon Msuva
Kpah Sherman
Coutinho

SIMBA:
Ivo Mapunda
Nassor Chollo
Mohammed Hussein
Hassan Isihaka
Juuko Murishid
Jonas Mkude
Rama Singano
Awadh Juma
Elius Maguri
Simon Sserunkuma
Emmanuel Okwi

ERASTO NYONI NDIYE MWANASOKA BORA WA TUZO ZA TASWA…..

5

Erasto nyoni akipokea tuzo yake….
1
Francis Cheka akipokea tuzo ya bondia bora kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Mecky Sadick
2
3
Rais wa TFF Jamal Malinzi akimkabidhi tuzo mchezaji bora  wa mchezo wa gofu
4
Mshambuliaji wa Azam FC Kipre Tchetche akipokea tuzo ya mwanasoka bora wa kigeni..
6
7
Feisal Pinto pia alikuwepo…….
8
Watangazi Enock Bwigane ( TBC ) pamoja na Sauda Mwilima ( STAR TV )
9
Mkurugenzi wa Radio One Deo Rweyunga akimkabidhi mjumbe wa kamati ya utendaji ya RT bwana Tullo Chambo tuzo  kwa niaba ya mwanariadha bora.
Capture
kutoka kushoto ni Rais wa TFF Jamal Malizi , Mkurugenzi wa wizara ya michezo ndugu Leonard Thadeo pamoja na Mahmoud Zubeiry mmiliki wa blog ya  Binzubeiry.

MAMBO YA WATANI NDIO YAMEANZA KABLA YA UWANJANI TAIFA

MOJA YA MAGARI YALIYOKATIZA MTAA YA JIJINI LA DAR ES SALAAM, LEO LIKIWA LIMEPAMBWA KWA RANGI ZA YANGA. HII INAASHIRIA LEO NI SIKU YA WATANI HASA, YANGA NA SIMBA WANAOKUTANA KWENYE UWANJA WA TAIFA KATIKA MECHI YA KIRAFIKI. KAZI IPO.