MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

Tuesday, 3 May 2016

IGP Mangu: Sina Taarifa Juu ya Agizo la Rais Kumpandisha Cheo Askari

  Amesema hajapewa taarifa za Rais Magufuli kuagiza koplo Deogratius Mbango kupandishwa cheo baada ya kumdhibiti mke wa mmoja wa mawaziri wa serikali yake kwa kosa la kukiuka sheria za usalama barabarani." Bado hajapandishwa cheo kwa sababu sijapewa taarifa hizo...

Urusi Sasa kujikita Tanzania, yapanga Kujenga Mtambo wa Nyuklia Tanzania

   Makampuni makubwa ya Viwanda na uzalishaji ya Kirusi ya "Russian Helicopters", "United Aircraft Corporation (UAC)" na "United Wagon Company (UWC)" yako tayari kuwekeza kwenye miradi ya viwanda nchini Tanzania.Waziri wa viwanda wa Urusi amesema Urusi iko tayari...

Uchumi wa Tanzania Waongoza Afrika Mashariki Ukifuatiwa na Kenya

Tanzania inatarajiwa kusajili kiwango cha juu zaidi cha ukuaji wa uchumi wake mwaka huu katika kanda ya Afrika Mashariki na kati. Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya shirika la fedha la kimataifa - IMF. Katika ripoti yake iliyotolewa jana Tanzania inatarajiwa kusajili...

Mawaziri Waja juu Jeshi kuhusishwa na Siasa

  MAWAZIRI wa Serikali ya Awamu ya Tano wamewajia juu wabunge wa upinzani na wananchi wanaovishutumu kila mara vyombo vya ulinzi nchini na kuwataka kuacha kuvihusisha vyombo hivyo na masuala ya kisiasa. Mawaziri hao ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,...

Polisi wawili watuhumiwa kuomba rushwa milioni 7.2/

POLISI mkoani Rukwa inawashikilia askari wake wawili wa Kituo Kikuu cha Polisi wilayani Nkasi, wakituhumiwa kuomba na kupokea rushwa ya zaidi ya Sh milioni 7.2 wamsaidie mtuhumiwa. Kaimu Kamanda wa Polisi wa Rukwa, Leonce Rwegasira alitaja askari hao kuwa ni Konstebo...

Monday, 2 May 2016

Mamlaka ya Bandari-TPA Yataja Sababu Iliyosababisha Mizigo Bandarini Dar es Salaam Kupungua

Siku moja baada ya serikali  kuziagiza mamlaka ya Bandari-TPA, na Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, kufanya uchambuzi wa kina ili kubaini sababu za kupungua kwa shehena ya kontena zinazoingia nchini kupitia Bandari ya Dar es salaam kwenda nchi jirani, Kaimu Mkurugenzi...

Masoud Kipanya Aitaja Sababu iliyomrudisha Clouds FM

Masoud Kipanya amerejea tena Clouds FM baada ya miaka minane kuondoka. Mchoraji huyo maarufu wa katuni ya Kipanya, anasikika kwenye kipindi cha Power Breakfast. “Sijui kama unajua kuwa mimi Clouds nilifukuzagwa kazi! Msingi wa kutoka Clouds ni kwamba sikutoka kwasababu...

Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein Aapishwa Rasmi Kuwa Mjumbe wa Baraza la Mawaziri

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein leo asubuhi tarehe 02 Mei, 2016 ameapishwa kuwa mjumbe wa Baraza la Mawaziri ili aweze kushiriki na kutekeleza majukumu yake ndani ya Baraza hilo. Rais Shein ameapishwa na Jaji Mkuu...

Mahakama ya Kisutu Yatoa Hati ya Kukamatwa kwa Meya wa Kinondoni, Boniface Jacob

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar imetoa hati ya kukamatwa kwa Meya wa Kinondoni, Boniface Jacob (Pichani)kutokana na kutofika mahakamani. Meya huyo anakabiliwa na shitaka la kumshambulia  mwandishi wa Habari wa gazeti la Uhuru, Christopher Lissa na...

Bora Ukimwi Kuliko Kutumia Dawa za Kulevya-Ferooz

Msanii wa kizazi kipya Ferooz amefunguka na kusema ni bora mtu apate virus vya Ukimwi kuliko kutumia madawa ya kulevya kwani anadai mtu akitumia dawa za kulevya mwisho wake ni kuaibika na kushindwa kufanya mambo ya msingi katika jamii.Akizungumza kwenye kipindi cha eNewz...

Prof. Tibaijuka: Rais Magufuli Aache Kutumbua Majipu..Wengine Tunatolewa Kafara na Mtandao Hauguswi

Akiongea na Count Down ya Clouds Fm Prof Tibaijuka amesema yeye ni muhanga wa ufisadi. Amesema kuna mtandao wa mafisadi unaotoa watu kafara na wenyewe hauguswi."Naafiki kuanzishwa kwa mahakama ya mafisadi, labda itasaidia kukamatwa na kushitakiwa mafisadi wenyewe....

Zitto: Millioni 50 za Magufuli Kila Kijiji ni Hadaa Kwa Wananchi.

  MBUNGE wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe, amesema Serikali ya Awamu ya Tano imewahadaa wananchi kuhusu kuwapa Sh. milioni 50 kila kijiji/mtaa huku akiamini ahadi hiyo haitekelezeki.Zitto alisema ahadi hiyo "kimahesabu, haitekelezeki.""Kwanza kwenye...

Meya wa Kinondoni Agawa Bure Maeneo ya Biashara Leo na Kufuta Umiliki wa Vibanda na Vizimba 100

  Meya wa Manispaa ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam Mstahiki Boniface Jacob amezua taharuki kwa wamachinga wa ubungo na kukimbia biashara zao wakiambatana naye mithili ya Maandamano mara baada ya kutangaza kufuta umiliki wa vizimba na mabanda takriban 100 yaliyokuwa...

Baada ya Kutoka Marekani Mtoto Getrude Clement Akaribishwa Bungeni Leo

Getrude Clement mwenye umri wa miaka 16 ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha tatu anayesoma shule ya Sekondari Mnarani iliyopo jijini Mwanza, leo amepata nafasi ya kufika bungeni Dodoma baada ya kupewa mwaliko wa Serikali  Hivi karibuni Getrude  alihutubia...

Nyumba 400 Zabomolewa Eneo la Iloganzila Jimbo la Kibamba Jijini Dar es Salaam

  Wakazi waliojenga eneo la Iloganzila Jimbo la Kibamba Dar es salaam leo wamebomolewa nyumba zao ambazo ni zaidi ya nyumba 400, zoezi hilo limekuja baada ya amri iliyotolewa na Mahakama Kuu juzi. Taarifa zinasema eneo hilo lenye ukubwa wa heka 33, mali ya Henry Kashangaki...