MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

Tuesday, 5 January 2016

Taarifa Muhimu Kwa Umma Kutoka TAMISEMI


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Boniface Simbachawene (Mb) kwa Mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu cha 2(2) cha Amri ya kuanzisha Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), (The Executive Agencies) (The Dar Rapid Transit Agency) (Establishment) Order ) Tangazo la Serikali  namba 120 la 2007, amemteua Mhandisi Ronald Lwakatare kuwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka Dar es salaam (DART) kuanzia tarehe 04/01/2016.

Uteuzi huo unafuatia kusimamishwa kazi kupisha uchunguzi kwa aliyekuwa Mtendaji Mkuu Bibi Asteria L. Mlambo tarehe 23/12/2015.

Kabla ya uteuzi huu, Mhandisi Ronald Lwakatare alikuwa Naibu Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Mfuko wa Barabara (Road Fund Board) akishughulikia Ufuatiliaji na Tathmini. Mhandisi Lwakatare anatakiwa kuripoti na kuanza kazi mara moja.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini cha Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Januari 05, 2016

Mama Samia Nae Ameanza Kazi Rasmi ......KATEMA CHECHE Jana Baada ya Kutua Geita.

Makamu wa Rais wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan jana jioni aliwasili  mkoani Geita  na akakutana na uongozi wa mkoa huo ambapo alisisitiza suala la  wananchi kunufaika na mgodi wao wa dhahabu wa Geita Gold Mine.…

"Wakati nilipopita kwenye kampeni nilipita kwenye mgodi wa Geita Gold Mine nikaangalia hali ya watu wa Geita nikawa na majonzi makubwa…sikuridhika kuwa na mgodi mkubwa kama ule na hali ya watu wa Geita iko ilivyo hivi nikawa sikuridhika nilikuwa mkali kidogo." Alisema Mama Samia  na  kuongeza;

"Wakati naangalia presentation nimeona amount nzuri kidogo inatolewa kwenda kwa watu ingawa bado ninamaswali yangu ambayo nitayafanyia kazi ili tuone ni kiasi gani sahihi kinatakiwa kutolewa na mgodi kwenda kwa wananchi, dhahabu iliyopo niyawana Geita Mungu amewaumbia katika ardhi yao

"Hatukatai kuwa na wawekezaji wachimbe lakini uchimbaji uwe na faida kote wao wapate na wananchi wapate kwa hiyo hatunabudi kusimamia vizuri na kuhakika kwamba wananchi wa Geita wanafaidika na rasilamali ambayo Mwenyezi Mungu amewapangia."
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa Geita Mhe. Fatma Mwassa wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa GGM Mkoani Geita jana Januari 04,2016 kwa ajili ya kuanza ziara ya siku mbili ya kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo Mkoani humo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na baadhi ya wawekezaji wa Mgodi wa GGM Mkoani Geita alipowasili Uwanja wa ndege wa GGM Geita jana Januari 04, 2016 kwa ajili ya kuanza ziara ya siku mbili ya kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo Mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa Geita Mhe. Fatma Mwassa akizungumza wakati akitoa Taarifa ya Maendeleo ya Mkoa wa Geita, kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia), katika kikao kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo, jana Januari 4, 2016. Katikati ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Injiani Gerson Lwenge.

Wahispania Wagundua Tiba ya UKMWI



Wakati dunia ikiwa na zaidi ya watu 34 milioni wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (VVU), madaktari nchini Hispania wametangaza kugundua tiba ya ugonjwa huo wanayodai ni uhakika.
Kwa kutumia damu ya kupandikiza kutoka kwenye kitovu mwana (umbilical cord) cha mtu ambaye ana vinasaba ambavyo havipokei virusi hivyo vya Ukimwi, wataalamu hao wa tiba wa Hispania wanaamini kuwa wanaweza kutibu ugonjwa huo baada ya mafanikio waliyopata kwa mgonjwa mmoja.
Madaktari hao wa Kitengo cha Taifa cha Upandikizaji (ONT) cha Hispania walichukua damu ya vitovu mwana vya watu wenye vinasaba ambavyo havipokei VVU na kuipandikiza kwa mtu anayeishi na virusi hivyo. Baada ya miezi mitatu, mgonjwa huyo alipimwa na kuonekana hana virusi.

Daktari wa Programu ya Upandikizaji kutoka Taasisi ya Tiba ya Catalan, Barcelona, Rafael Duarte alisema mgonjwa aliyetibiwa kwa njia hiyo, Timothy Brown (37), alikuwa anaishi na VVU tangu mwaka 2009 na madaktari hao walithibitisha kuwa amepona baada ya kupandikizwa damu hiyo.

Mgonjwa mwingine aliyefanyiwa majaribio ya tiba hiyo alipona VVU, lakini miaka mitatu baadaye alifariki kwa ugonjwa wa saratani.

Timu ya madaktari wa Hispania ililiambia gazeti la kila siku nchini humo la El Mundo kuwa wana uhakika kuwa wameleta mapinduzi katika mapambano ya Ukimwi na magonjwa yanayofanana na hayo.

Dk Duarte alisema mwaka 2015 umekuwa wa kujivunia ugunduzi huo mkubwa duniani, ingawa alitahadharisha kuwa tiba kamili haiwezi kupatikana katika siku za usoni.

Kaimu mkurugenzi wa mwitikio wa Taifa wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (Tacaids), Dk Morris Lekule alisema utafiti kama huo hauna budi kufuata taratibu zote na kuthibitishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) kabla ya kutangazwa kuwa ni tiba sahihi.

“Kila mara taarifa zinakuja zikisema tiba ya Ukimwi imepatikana, lakini tiba kupata uthibitisho kwamba ni sahihi, ni mchakato mrefu unaotakiwa kuhakikisha kama kweli dawa hiyo inatibu na ni lazima WHO wathibitishe hilo,” alisema.

Alisema ni vizuri kama wataalamu hao wakapata uhakika kutoka WHO badala ya kuwapa watu matumaini kuwa kuna tiba na baadaye matumaini hayo yanapotea.

Daktari wa kitengo kinachoshughulika na masuala ya Ukimwi cha WHO, Richard Banda alisema hana taarifa za tiba hiyo. Tiba inavyofanya kazi Madaktari wa ONT walitumia damu ya mtu mwenye vinasaba vya ‘CCR5Delta’ ambavyo seli zake haziathiriwi na virusi hivyo vya Ukimwi.

Dk Duarte alisema kwanza huziua seli za damu ya mgonjwa kwa kutumia mionzi halafu seli mpya (kutoka kwenye damu ya mtu mwenye seli zisizoathiriwa na VVU hupandikizwa. Damu hiyo ilipandikizwa kwa mgonjwa mwenye virusi hivyo na saratani ya damu.

Baada ya seli hizo kupandikizwa, Virusi vya Ukimwi vilivyo kwenye damu ya mgonjwa hushindwa kujipenyeza katika seli mpya zilizopandikizwa. “Siku 11 baada ya upandikizaji, mgonjwa wa Barcelona alianza kupata nafuu na baada ya miezi mitatu, tulimpima na kukuta hana VVU,” alisema.

Zitto: Rais Magufuli Ameshaipotezea Nchi Mapato ya Bilioni 8 Tangu Aingie Madarakani

Mbunge wa Kigoma mjini, Zitto Kabwe ameilalamikia serikali ya Magufuli kwa kitendo chake cha kukaa kimya kuhusu ufisadi unaoendelea kufanywa na Harbinder Singh Seth, mmiliki wa IPTL, ambaye huvuna kiasi cha malipo ya bilioni 4 kila mwezi kama malipo ya kuliuzia umeme shirika la ugavi wa umeme nchini, Tanesco.


Zitto ambaye ni mmoja wa wabunge walioibua na kusimamia kidete sakata la ufisadi wa Tegeta Escrow bungeni mwishoni mwa mwaka juzi (2014), amesema hayo kufuatia tangazo la serikali kuhusu kashfa ya Commodity Import Support ya miaka ya miaka 1980 na 1990s, ambapo ameisifu serikali kwa hatua hiyo na kuhoji iweje ikomae na kashfa hiyo tu, huku ikisita kuchukua hatua kwenye sakata la IPTL linaloigharimu serikali kiasi kikubwa cha fedha kila mwezi isivyostahili?

Kampuni ya IPTL imeshalipwa fedha mara mbili tangu Rais Magufuli aingie rasmi madarakani, hivyo kufanya hesabu zitimie bilioni 8 kwa kipindi cha miezi miwili mpaka sasa.

Msome;

"Nimeona tangazo la Serikali kuhusu kashfa ya Commodity Import Support. Hii ni kashfa ya miaka ya 1980s na 1990s. Ni hatua nzuri. Lakini ina maana gani wakati Serikali inavuta miguu kwenye suala la IPTL? Harbinder Singh Seth na genge lake wanavuta tshs 4bn kila mwezi. Kwa kutochukua hatua kuhusu IPTL, Rais Magufuli ameshaipotezea nchi mapato ya tshs 8bn tangu aingie madarakani. ‪#‎TegetaEscrow‬ ndio baba la mtandao wa ufisadi nchini kwetu" - Zitto Kabwe.

Rais Magufuli Alidanganywa na Huyu Mgonjwa Hospitali ya Muhimbili...Mazito yaibuka


DAR ES SALAAM: Yule mgonjwa anayeaminika ndiye aliyetoa siri ya kuharibika kwa mashine za CT Scan na MRI Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa Rais Dk. John Magufuli na wiki iliyopita kudai amelazwa chini, Chacha Makenge, amesababisha mapya kuibuka.

Wakizungumza na gazeti hili mwishoni mwa wiki iliyopita, maofisa uhusiano wa Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (Moi), Frank Matua na Patrick Mvungi kwa nyakati tofauti, walisema kuwa, mgonjwa huyo hakuwa na tatizo lolote la kiafya na alisharuhusiwa kuondoka hospitalini hapo.

“Alipimwa, tena alikuwa mgonjwa wa kwanza kupimwa kwenye CT Scan baada ya kutengenezwa na kugundulika uti wake wa mgongo uliumia miaka mitatu iliyopita. Alipoulizwa alikiri kuumia Stakishari… Kwanza haiwezekani mgonjwa wa uti wa mgongo kumlaza chini,” alisema Matua.
Akaongeza kuwa, baada ya kuonekana hana tatizo, aliruhusiwa kwenda nyumbani lakini anakataa akidai hana pa kwenda. Ndipo alipowaeleza maofisa hao kuwa ana familia ipo Mugumu, Serengeti mkoani Mara.


“Tulimtafutia tiketi ya basi na fedha za matumizi ili aende kwao lakini siku ya safari alikataa kwenda akisema anakwenda msibani. Pia akaelekeza kuwa fedha tulizomtengea kwa safari wapewe wagonjwa wengine ziwasaidie.

“Baada ya siku kadhaa, akarudi hapa Moi. Tulipomkumbusha kuwa amesharuhusiwa, alikataa kuondoka, hatukumshusha kitandani.

Wagonjwa wanaokataa kwenda makwao baada ya kuruhusiwa hapa hospitali wapo wengi na hatuwafukuzi, in humanitarian ground (kibinadamu), tunawapa huduma zote za chakula na malazi kwa gharama za serikali hadi utaratibu mwingine utakapofanyika,” alisema Matua.
Alifafanua kuwa, baada ya kuona Chacha anawasumbua kwa tabia zake mbalimbali, walimchunguza, wakagundua alishawahi kuwa na jalada katika wodi ya wagonjwa wenye matatizo ya akili Muhimbili, hivyo sasa wanafanya utaratibu mwingine wa kumsaidia.

Wiki iliyopita, gazeti hili lilikwenda Muhimbili, Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (Moi) na kumkuta Chacha akiwa amelala chini na akadai ameshushwa kitandani.

Kwa kuona kuwa uwepo wake pale unaweza kusababisha kumchafua Rais Magufuli aliyesimamia zoezi la kupatikana kwa vitanda, gazeti hili liliandika habari zake ili uongozi wa hospitali hiyo uchukue hatua bila kujua kwamba huko nyuma mgonjwa huyo aliwahi kufunguliwa jalada kwenye wodi ya wagonjwa wa akili.

Hata hivyo, maofisa uhusiano wa taasisi hiyo hawakupatikana wakati huo kuzungumzia tukio hilo lililowaacha midomo wazi watu walioingia wodini humo siku hiyo ya tukio.

Wananchi Watumia Mabango Kufikisha Ujumbe Kwa Rais Magufuli

 

 

Wakati muda wa `mapumziko’ ya bomoabomoa ukimalizika leo huku jaribio la kupata zuio la muda likiwa limewekwa kiporo, wakazi wa Jangwani ambako nyumba zitaanza kubomolewa leo, jana waliweka mabango barabarani yanayotuma ujumbe wa aina mbalimbali kwa Rais John Magufuli.

Bomoabomoa hiyo ilianza Desemba mwaka jana likilenga nyumba zilizojengwa kwenye Bonde la Mto Msimbazi, lakini lilisitishwa kwa siku 14 na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi hadi Januari 5, mwaka huu kuwapa nafasi wakazi kuondoka kwa hiari yao kuokoa mali zao.

Wakazi wa Jangwani walitumia mwanya huo wa kusitisha ubomoaji, kufungua kesi Mahakama ya Ardhi kupinga kuondolewa maeneo hayo bila ya kupatiwa sehemu nyingine na kuwasilisha ombi za zuio la ubomoaji, lakini chombo hicho cha sheria kilikataa kubariki mambo hayo ya kutaka sitisho la bomoabomoa liendelee wakati kesi ikiendelea mahakamani.

Wakati wawakilishi wa wakazi hao wakiwa mahakamani katikati ya jiji, watumishi wa halmashauri za jiji waliendelea kuweka alama nyumba zinazotakiwa kubomolewa wakiwa wamesindikizwa na ulinzi mkali wa polisi.

Hakukuwepo na wakazi waliojitokeza kuzuia uwekaji alama hiyo ya “X” inayotaarifu kuwapo kwa ubomoaji, lakini mabango ya maboksi yaliyosimikwa kwenye vifusi na maeneo mengine ya jangwani, yanatosha kuelezea hisia za wakazi hao wanaoishi maeneo ambayo yametangazwa kuwa hatarishi.