WAKATI wachezaji wengine wanavuna fedha za usajili katika kipindi cha kuelekea dirisha kuu la uhamisho, Mrisho Khalfan Ngassa ambaye yumo ndani mkataba na klabu yake, Yanga SC naye amevuna mamilioni kimtindo mwingine.
Kwa pamoja, Ngassa na mchezaji wa Yanga SC na timu ya taifa, Taifa Stars jana wamefanya tangazo la magodoro ya Comfy, ambayo yamewafanya wavune mamilioni.
Kiasi gani wamepata? Siri yao, lakini mbali na wao, mshambuliaji wa timu ya taifa ya wanawake, Twiga Stars, Mwanahamisi Omary ‘Gaucho’ na winga wa Simba SC, Ramadhani Singano ‘Messi’ nao pia wameshiriki tangazo hilo kwa pamoja mwigizaji Ahmed Ulotu ‘Mzee Chilo’.
![]() |
Dili la mahela; Mrisho Ngassa kulia akiwa Deo Munishi 'Dida' katika na Mwanahamisi Omar 'Gaucho' na godoro la Comfy baada ya kumaliza kufanya tangazo la bidhaa hiyo |
![]() |
Watu pesa; Kulia kabisa Mzee Chilo ambaye naye ameshiriki tangazo hilo |
Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment