Kutoka Kalenga: Uchaguzi wa Ubunge - Machi 16, 2014
Wakuu kumekucha salama, hali ni yautulivu,CHANZO JAMMII FORUUM
Vituo vyote 230 na kata zote 13 tayari vimefunguliwa, Mawakala wa Chadema tayari wamesharipoti vituoni,
Kituko nikuwa Mwigulu asubuhi hii analindwa na polisi wenye silaha kali akiwa na msafara wa magari sita utafikiri ni rais wa nchi, sijui analindwa hivi kama Mkuu wa Green Gurd au Naibu waziri?
Ulinzi kwa upande wa Chadema umeimarishwa kama tupo Kokrovu vile, hata akatize nzi tu lazima asimamishwe na kukaguliwa.
Katika kituo cha Nzihi watu wanaoaminika kuwa ni mabarozi wa ccm wamefika nakuanza kuleta fujo, Vikosi imara vya Red Brigade vya chadema vimewatia nguvuni na polisi wakaja nakuwatia pingu mabalozi hao wawili na wakachukua mizoga yao,
Mambo mengine ni shwari kabisa hakuna uvunjifu wa amani,
Tulia upate zaidi toka uwanja wa ukombozi
UPDATES
- Wale waliopata ajali jana ambao ni Kimaro mwenyekiti wa ccm arusha mjini kwa ajali ya jana kavunjika bega,majeshi kavunjika mbavu na shingo,hawapo kabisa kwenye uwanja wa vita.
- Chopa ya Chadema ipo angani muda huu ikiwa na mgombea, mwenyekiti taifa na maafisa usalama kadhaa wa Chadema, itatua kata zote 13, na vituo vyote 230 vitakaguliwa
- Vikosi vya ulinzi vya chadema vinamshikiria gamba mmoja aliyekuwa kakamatwa asubuhi na kukabidhiwa kwa polisi lakini karudi tena kuja kufanya fujo, Red Brigade imeamua kumshikilia akae hapohapo kituo cha kupigia kura akiwa chini ya ulinzi mpaka uchaguzi uishe ili kuepusha vurugu. Pongezi kwa Red Brigade!!
- Misururu ya wapiga kura ni mirefu wengi wao ni akina mama na vijana. Kila uso unaouna unajieleza wenyewe kuwa utapiga kura kwa Mama Grace Tendega,
- Zoezi la upigaji kura linaendelea, watu wamejitokeza wengi, inatia moyo sana kwa mwamko huu,
- Vikosi vya usalama vya Chadema vimekamata watu wawili wakiwa na vitambulisho vya polisi.
- Wamechezea kichapo mno kisha kudhitibiwa mpaka uchaguzi uishe!
========
Mdau huyu anasema,
UPDATES
Kituo Kalenga A wapiga kura 422, waliohakikiwa 288 waliojitokeza hadi sasa 13:26 ni 146. Kwa mujibu wa msimamizi
UPDATES
Wakuu, Mbunge wa Chadema aliyetekwa na kupigwa na kudharirishwa na ccm,
Mama Rose Kamili hali yake si nzuri na muda wowote anaweza kuletwa na helkopta KCMC kwa matibabu zaidi,
Tumuombee kwa Jah apone haraka na haki itendeke kwa wahalifu hao,
UPDATES:
Kituo Lukwambe kata Ulanda waliojiandikisha 299 mpaka 15.05 wamepiga 154
.............................. ......
VITUO VYAKUPIGIA KURA VIMEFUNGWA RASMI, WANAORUHUSIWA KUENDELEA KUPI KURA NI WALIOPO KWENYE FOLENI TU.
Shughuli za uhesabuji kura zitaanza mda wowote kuanzia sasa!
MATOKEO:
No comments:
Post a Comment