MPANDA PIKIPIKI AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI MKOANI MBEYA.
MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA BONIPHACE MWALUM (43)
MWENDESHA PIKIPIKI, MKAZI WA ILONGO WILAYA YA MBARALI ALIFARIKI DUNIA
MUDA MFUPI BAADA YA KUFIKISHWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA KWA MATIBABU
BAADA YA KUGONGWA NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI IT 5239 AINA YA TOYOTA CALDINA LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA AMIRI MUGASA (44) MKAZI WA TABATA JIJINI DAR-ES-SALAAM. TUKIO HILO LILITOKEA MNAMO TAREHE 20.02.2014 MAJIRA YA SAA 11:00HRS ASUBUHI
KATIKA BARABARA KUU YA MBEYA/NJOMBE. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI WA
GARI, DEREVA AMEKAMATWA NA TARATIBU ZA KISHERIA ZINAENDELEA DHIDI YAKE.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI ROBERT MAYALA
ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA
KUFUATA/KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA UASALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA
AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA WATEMBEA KWA MIGUU
KUZINGATIA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI IKIWA NI PAMOJA NA KUTEMBEA
PEMBEZONI MWA BARABARA NA KUVUKA SEHEMU YENYE VIVUKO YAANI ZEBRA
CROSSING ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA KWA KOSA LA KUJERUHI.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA GEOFREY EDSON (16) MKAZI WA ILEMI JIJINI MBEYA BAADA YA KUMJERUHI KWA KUMCHOMA KISU TUMBONI JASTINE ASAJILE (19) MKAZI WA MAKUNGULU. TUKIO HILO LILITOKEA MNAMO TAREHE 20.02.2014 MAJIRA YA SAA 16:30HRS JIONI
HUKO KATIKA KILABU CHA POMBE. CHANZO NI UGOMVI ULIOTOKEA BAINA YAO
WAKIWA WAMELEWA POMBE KWENYE KILABU CHA POMBE ZA KIENYEJI KIITWACHO
MBAGA. MHANGA AMELAZWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA NA HALI YAKE INAENDELEA
VIZURI. MTUHUMIWA AMEKAMATWA NA TARATIBU ZA KISHERIA ZINAENDELEA DHIDI
YAKE. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI ROBERT MAYALA
ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUNYWA POMBE KUPITA KIASI KWANI NI HATARI
KWA AFYA ZAO. PIA ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTEMBEA NA SILAHA KATIKA
SEHEMU ZA STAREHE KWANI NI KINYUME CHA SHERIA.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WAFANYABIASHARA WATANO WAKIWA NA BIDHAA ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI NA ZILIZOISHA MUDA WAKE.
KATIKA OPERESHENI INAYOENDESHWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA KUSHIRIKIANA NA MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA [TFDA] MKOA WA MBEYA, JESHI LA POLISI LINAWASHIKILIA WAFANYABIASHARA WATANO 1. JENIPHER SANGA (25) MKAZI WA SOWETO, 2.SHUKURANI AMBILIKILE (18) MKAZI WA IYUNGA, 3. ASWILE ASUKILE (31) MKAZI WA AIRPORT, 4. MEGU AMOS (28) MKAZI WA IYUNGA NA 5. OSEAH JOHO (32)
MKAZI WA ISANGA WAKIWA NA BIDHAA ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI NA
ZILIZOISHA MUDA WAKE WA MATUMIZI. WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 20.02.2014 MAJIRA YA SAA 12:30HRS MCHANA WAKIWA NA POMBE KALI KONYAGI CHUPA NDOGO 48, KONYAGI CHUPA KUBWA 04, KONYAGI VIROBA BOKSI 66 NA POMBE KALI AINA YA VALUE CHUPA 23. TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI ROBERT MAYALA
ANATOA WITO KWA WAFANYABIASHARA KUACHA KUUZA/KUSAMBAZA BIDHAA
ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA. PIA ANATOA
WITO KWA WAFANYABIASHARA KUACHA KUUZA BIDHAA ZILIZOISHA MUDA WAKE WA
MATUMIZI KWANI NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANATOA RAI KWA
YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MTU/WATU WANAO JISHUGHULISHA
NA UUZAJI/USAMBAZAJI WA BIDHAA ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA ZILIZOISHA MUDA
WAKE AZITOE KWA JESHI LA POLISI AU KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE
NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO, VINGINEVYO WAJISALIMISHE
WENYEWE.
SIGNED BY:
[ROBERT MAYALA – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment