Mwandishi maalum wa www.matukiodaima.com Katavi
Katika
kukabiliana na vitendo vya ujangili vinavyoendelea kushika kasi ndani nan je ya
mipaka ya nchi yetu, Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) litaendeshwa katika
mfumo wa jeshi-usu katika siku chache zijazo ambapo watumishi wake watalazimika
kupitia katika mafunzo maalum ya kijeshi.
Mkurugenzi
Mkuu wa TANAPA aliyasema hayo mwishoni mwa wiki alipokuwa akifunga rasmi
mafunzo ya askari wapya 96 walioajiriwa na TANAPA na kuhudhuria mafunzo ya miezi
minne katika Hifadhi ya Taifa Katavi mwishoni mwa wiki.
Kijazi alisema kuwa TANAPA
imeanzisha utaratibu mpya ambapo sasa askari wanaoajiriwa na shirika kutoka
katika Vyuo vya Wanyamapori vya Mweka na Pasiansi pamoja na wale wa kutoka
Jeshi la Kujenga Taifa watalazimika kupitia mafunzo maalum yanayoandaliwa na
shirika kwa ajili ya kuwawezesha waajiriwa wapya kufahamu mazingira halisi ya
utendaji kazi katika eneo la uhifadhi katika maeneo ya Hifadhi za Taifa. |
No comments:
Post a Comment