WENGER AMTENGEA DI MARIA MAMILIONI, HOFU YA BALE YAZIDI KUMSOGEZA MLANGO WA KUTOKEA
Gareth Bale kutua
Real Madrid ni habari mbaya kwa Muargentina, Angelo Di María na Kocha Mkuu wa
Arsenal, Arsene Wenger ameweka wazi kuwa anamhitaji. Wenger tayari
ameweka dau lake kwua ni euro milioni 30 ameshatenga kwa ajili ya kumpata winga
huyo mwenye kasi.
Tokea mwanzo, Di
Maria alieleza kuwa atahitaji kubaki Madrid, lakini inaonekana hatakuwa na
namna kama Bale atakamilisha uhamisho huo leo au kesho kwa kuwa tayari yuko
Hispania.
Wenger naye
anaamini Di maria atakuwa msaada mkubwa katika kikosi chake ambacho kilianza
ligi kwa kipigo cha bao 3-1 dhidi ya Aston Villa kabla ya kuamka na kuichapa
Fulham kwa idadi kama hiyo.
No comments:
Post a Comment