Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limetangaza kutoa donge
nono la Shilingi milioni 100/= kwa mtu yeyote atakayewezesha kupatikana
kwa taarifa za kundi la uhalifu linalojihusisha na vitendo vya
kuwamwagia na kuwadhuru watu tindikali.
Kamanda wa Polisi Kanda
hiyo, Suleiman Kova amesema: “Nimeamua kuomba fedha hizi serikalini ili
nimpe mtu atakayewezesha kupatikana kwa taarifa hizo, hatimaye kukomesha
vitendo hivi. Kemikali hii imekuwa na madhara makubwa.”
No comments:
Post a Comment